Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi leo Oktoba 17, 2025 ametembelea Hifadhi ya Mkomazi, moja ya vivutio na hifadhi zenye zao la utalii wa Faru utakayemuona kwa karibu zaidi kuliko hifadhi nyingine nchini.
Mradi huo wa Faru hadi kufikia Septemba 2025 kuna jumla ya Faru Weusi 50 (Madume 22 na majike 28).
Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara na hata malazi katika hifadhi hiyo inayoweza kufikika kirahisi kupitia Wilaya ya Same lakini pia unaweza kuingilia Mwanga na maeneo mengine yenye mageti ya hifadhi hiyo ya kimkakati.