Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Bw. Nkoba Mabula, akikagua Banda la Maonyesho ya Kitaalam katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) mkoani Kilimanjaro, wakati wa Mahafali ya 28 ya chuo hicho. Mazao mbalimbali ya misitu yaliyowasilishwa ni kielelezo cha mnyororo mzima wa thamani unaotokana na rasilimali za misitu na yanawakilisha sehemu ya mafunzo kwa vitendo yaliyotekelezwa na wahitimu wa ngazi ya Astashahada na Shahada kwa mwaka 2025